Jinsi ya Kuishi Maisha Kama Mkristo

Vile tulisema pale mwanzo kwa kitabu hiki Mkristo ni mtu ambaye ameamua kuishi maisha ya kumfuata Yesu na mpango wake kwa maisha yetu. Kuna njia mbili ya kujifunza kufanya hivi:

Mzabibu na Matawi

Ni vigumu kuchagua mojawapo hata chache ama mafundisho ya Yesu kuwa mazuri zaidi ama ya muhimu sana kusoma. Injili ya Yesu kwa mlima wa Msaituni (ambapo anafundisha mambo yanayoitea heri- Mathayo 5 na Luka 6) ni kifungu watu wengi wanakijua kama wanajua mafundisho ya Yesu yeyote. Nimezoea kifungu katika kitabu cha Yohana.

Upendo Mkuu wa Aina Hii

Baada ya kuongoka kwake Kwa miujiza Paulo wa Tarso alikuwa mhubiri aliyefikia watu wengi pia alikuwa mwandishi mashuhuri. Kwa barua yake Kwa wakristo walioishi Korintho (Ugiriki) alionyesha mtindo wa kutojipenda hii Ni tabia ambayo inafaa kuwa na kila Mkristo.

Kubadilisha Mawazo Yetu

Paulo anatuambia katika kitabu cha Warumi (12:2) tusifanane sura ya dunia lakini tubadilishwe kwa kuhuisha mawazo yetu. Katika barua yake kwa wakristo walioko Filipi (Ugiriki) alituonyesha vile tutatimiza hili:

Matunda Ya Roho

Katika Yohana 15 Yesu anasema kuhusu kumtii ndio tukaweza kuzaa matunda mengi. Katika barua yake kwa Wakristo walioko Galatia (mjii sasa unaitwa Uturuki) Paulo anaonyesha dhamira ya watu ambao wamejitolea kuishi katika roho:

Kusudi la shida

Yesu alitufundisha na barua zote za mitume zinatibitisha kuwa lazima tutarajie shida katika maisha yetu; kuwa mkristo sio ngao ya kuebuka na shida watu hupitia katika maisha. Katika kitabu cha Yakobo anatupa mtazamo mpya wa kuona shida zetu. Wanaweza kuwa ni nafasi kubwa ya kukua.

Kukua katika Imani yako

Mitume Petro aliandika barua mbili ambazo zimenakiriwa katika agano jipya. Katika barua yake ya pili anainyesha jinsi na mwenendo wa kukua Imani kwa Mungu.