Mwisho wa Hadithi

Hata kama ni majaribu aina gani tunayoyapitia kwa sababu ya kuwa mkristo tuko na hakikisho kubwa kujua kuwa Mungu yuko ushukani wa hadithi. Anajua mwisho wa hadithi ndio maana ni jibuko la furaha.
Kitabu cha Ufunuo
Kitabu cha ufunuo ni rekodi ya maono yaliyopewa mitume yohana alipokuwa katika utumwa katika kisinga cha Ugiriki ya patimo. Kinawezakua kitabu kigumu Zaidi katika bibilia kusoma. Kitabu cha ufunuo kiliandikwa wakati wa dhiki kuu kwa wakristo. waandishi wengine wanaamini kuwa Yohana alikiandika kwa njia ambayo wakristo wasomi wangeelewa. Wengine wanaamini kuwa maono mengi kama sio yote Yamekwishatimia.
Lakini kama manabii wa agano la kale. Yohana amekuwa akiyaona mambo yatakayokuja, kwa mfano Shetani jimbuko la uovu katika dunia anachukulia kuwa ameshinda milele kwa sababu kuna bado uovu duniani unabii huo hujatimia bado.
Hata kama ni vigumu kuelewa ishara na taswira katika ufunuo, unafaa kuisoma hata kama ni mara moja. Ufunuo wa Yohana 1:3 inaahidi Baraka kwa wale wanaosoma. Barua kwa makanisa saba yanazungumzia mengi kwa kanisa la kisasa. Na kama umesoma kifungu chochote kwa manabii wa agano la kale utapata ufanano kwa mtindo ya uandishi wa kutumia taswira na ishara inapendeza sana.
Kama hatujasoma chochote katika ufunuo ni vizuri tusome hata mlango wa mwisho. Mlango wa 22 kwayo tutapata tumaini kubwa kuhusu yale yanatungoja tutakapoenda nyumbani kwetu mbinguni.