Taifa La Israeli
Katika kitabu cha kumbukumbu la torati Mungu anawapa marsharti kwa kina kwa watu wake vile watakavyoishi watakapofika Kanani. Nchi Mungu alikuwa ameahidi Abrahamu. Hii ilijumuisha serikali watakayoiunda. Mwanzo wataongozwa na mfuatano wa waamuzi (kitabu cha Waamuzi) katika kitabu cha Waamuzi 17:14-15, Mungu akawaambia Waisraeli kuwa wafalme watawaongoza wana wa Israeli lakini wale wafalme ambao wamechaguliwa na kupakwa na Mungu.
Ijapo Sauli mfame wa kwanza wa Israeli alichaguliwa na Mungu alikuwa wa kutotii na kwa hali kubwa sana alikosa Imani. Mungu hakuendelea kuongoza Israeli kupitia kisasi cha sauli. (mwanawe jonathani hakurithi uongozi kutoka kwa babake). Vile tuliona pale mwanzo wa hiki kitabu vitabu vimepangwa kulingana na ujumbe vimebeba. vitabu vya kwanza vinane kutoka kitabu cha mwanzo mpaka Ruthu vinafanana na hadithi ya Mwanzo na vinafuatana hivyo kimiaka. vinafuatana vile matukia yalifanyika.
Hadithi ya taifa la Israeli imesemwa katia vitabu kadhaa katika agano la kale lakini sio kufuatana vile yalitukia, ili kuelewa nini kilichotokea kwa nani na kwa wakati gani ni vizuri tuwe na kitabu cha kurejelea kinachotoa wakati mambo yalitokea na wapi hizo hadithi zinawezapatikana katika agano la kale. Hapa tuna jedwali na ufupisho wa wafalme waliotawala Israeli na ni wapi hizo hadithi hupatikana katika agano la kale.
Tarehe za kukadiliwa | ||
(Wimbo uliobora, mhubiri na methali) | ||
Israeli ilitawanyika kuwa falme mbili. | ||
Mfalme Daudi
Mtu ambaye angekuwa mfalme na mfalme mkuu katika Israeli alitoka kwenye haikutarajiwa. Daudi alikuwa kijana mdogo zaidi kwa wote (sio wa kwanza vile ilikuwa kawaida) kwa mtu aliyeishi katika mji mdogo unaoitwa Bethlehem (inaonekana kawaida) ilikua kupitia kizazi cha Daudi yesu alizaliwa!
Kama kawaida ya wanaume wote ambao Mungu alikuwa amechagua kumsaidia kubeba mapenzi yake kwa dunia. Daudi hakuwa mkamilifu. Alifanya dhambi mbaya sana kwa wakati wake kama mfalme lakini bado katika kitabu cha 1 Samweli 13:14, Mungu amwambia nabii kuwa Daudi ni mtu anayetafuta roho ya Mungu.

Taifa Lisilotii
Mwanawe Daudi, Solomoni alichukua uongozi kutoka kwa babake kama mfalme. Solomoni alijulikana kuwa mtu amesoma sana na alikuwa amejawa na hekima. Huyu ndiye mfalme aliyewaongoza Israeli kukamilisha kujenga hekalu iliyoanzishwa na babake Daudi. Solomoni anapongezwa kwa kuandika vitabu viwili vya agano la kale; Wimbo uliobora, (Shairi la mapenzi) na kitabu cha Mhubiri.
Kama wakumbuka Mungu kwanza kuliko aliamuru watu wake kutokuwa miungi mingine. Cha kusikitisha ni kuwa Israeli ilisingirwa na mtaifa waliokuwa wanaabudu miungu mbalimbali na sanamu. Solomoni aliwaleta hawa watu wa kigeni kuja kusaidia kujenga hekalu pamoja na hao wafanyakazi walikuja na miungu yao. Kama vile tujuavyo ni vigumu kila wakati kuwa na watu ambao sio kama sisi na tuamini tofauti vile tunafanya, na tuzianze kuchukua baadhi ya Imani zao sana sana kama Imani yako iko kidogo. hii ndio ilifanyikia taifa la Israeli.
Solomoni alikuwa mfalme mkubwa kwa njia nyingi. Hata kama uongozi wake ulikuwa Katili kidogo. Aliweka ushuru mwingi kwa watu ili aweze kujenga hekalu pia ikulu ya anasa kwa sababu yake. Haya ndio baadhi ya mambo yaliyofanya taifa la Israeli kupasuka na kuwa na (taifa la Kaskazini(Israeli) na Kusini (Yuda).

Mungu atuma Maonyo Kupitia kwa Manabii
Taifa la Israeli lilichaguliwa na Mungu kuwa lake. lakini kwa wakati mwingi Waebrania walikuwa wanageuka na kuabudu miungu ya watu waliokuwa wanawazingira. Hii ibada ya miungu ilijumlisha mpaka kutoa kafara watoto wachanga na uasherati ambao Mungu hangevumilia kutoka kwa watu wake.
Mara kwa mara Mungu alituma manabii wake kuwaonya kuwa kutakuwa na kuadhibiwa kukali sana kwa kutotii. Kipengele cha mwisho katika agano la kale huandika mambo ambayo Mungu alihamasisha watu wake kuandika. Kila utabiri Mungu alifanya kupitia kwa watu wake kwa kushindwa na kupelekwa utumwani kwa Waisraeli ulikuja kutimia.
Ili kuona mpangilio wa maandishi ya manabii tunawezaiweka kwa jedwali linalofanana na lili tulitengeneza juu ya wafalme wa Israeli. matukio yaliyokua yakitendeka wakati wa Samweli wa kwanza na wa pili na wafalme wa kwanza na wa pili mambo ya nyakati ya kwanza na ya pili ni yale yale tu manabii walijaribu kuwaonya wana wa Israeli kwayo.
waebrania kutoka kusini kuwa utumwani | |||
Maombolezo | |||
Kiliandikwa utumwani | |||
Hagai, Zekaria | |||
Taifa Lililoshindwa
Vitabu vitatu vya mwisho wa Agano la kale; Hagai, Zakaria na Malaki, viliandikwa ili kuwatia moyo Wayahudi baada ya uahamisho na kuwafufua kwa Imani yao ya kitambokwa Mungu na kuwa waminifu tena katika kumwabudu Yeye (Uyaudi).

Baada ya mianzo ya bandia, waliweza kujenga hata hekalu jipya, ilikuwa ni kivuli tu kwa hekalu ya awali ya utukufu iliyojenygwa na mfalme solomoni lakini ilikua mahali katika nchi yao mahali wangemwabudu mungu mmoja wa ukweli tena.
Na vile manabii walikuwa wanatabili mwanguko waisraeli, unabii wao ulikuwa umechanywa pia na unabii kuhusu mwokozi, masii. mwenye atakuja kujenga agano jipya kati ya Mungu na watu wake.
Mungu aliwauliza watu walioshindwa kuwa wawe na Imani hata wakati vitu vilionekana kuwa vibaya Zaidi, kesho bado ilikuwa mikononi mwake na bao alitamani kuwa na uhusiano na mwanadamu kiumbe cha juu Zaidi.

Wakati Kabla na Baada Ya Yesu
Historia ina vipengele viwili, kabla yesu kuzaliwa na baada. miaka iliyo katika kalenda ni miaka tangu yesu kuzaliwa. tunaandika tarehe katika agano la kale na kitambulisho ya B.C inayomaanisha kuwa kabla yesu. tarehe baada ya yesu kuja ilitambulishwa na A.D ni ufupisha wa neno la kilatini "Anno Domini" maana yake "kwatika mwaka wa bwana wetu."
Kuna watu wasioamini kuwa yesu ni masii mwana wa Mungu mwenye anawezataka kutuchukua nche ya kuandika tarehe zetu wameanza kutumia B.C. inayomaanisha kabla ya majira ya kisasa. lakini majira yetu ya kisasa yanatambulishwa na yesu, wakati katika dunia kwahivya maana ni moja na vile tulisema awali. historia ina vipengele viwili, kabla yesu kuzaliwa na baada.

Uyahudi (Kumwabudu Mungu) Baada ya Utumwa
Kuabudu kwa wayahudi kulikuwa pamoja na kutoa dhabihu wanyama kwa msamaha wa dhambi zao. Kumbuka Mungu aliwambia Adamu na Hawa kuwa lazima watakufa kwa ajili ya dhambi zao kwa Wayahudi kutoa dhabihu kwa wanyama kwa Mungu vile aliwaamrisha. Ilikuwa ishara ya kubadilishana dhabihu ya uhai na dhambi zao.
Wakati wayahudi walirudi Israeli baada ya utumwa, tulisema kuwa manabii waliwahimiza watu kuanza kumwabudu Mungu na kutii amri zake zote.
Inaonekana kuwa Waebrania (angalau wale wachache ambao walirudi Israeli) mwishowe walipata adabu yao. Mungu hangeruhusu kuabudu kwa sanamu na kutotii. Wakuhani wa Wayahudi walioinuka na kuongoza wayahudi kama matokeo ya asili ya uongozi wao wa kiroho ilisaidia kutengeneza jamii iliyojisatiti kuwa aminifu. Hawakuruhusu wao wenyewe kuingiliwa na mitindo ya nje na walifanya bidi yao yote kutii kila herufi ya sheria zote za Mungu. Hii ndio jamii ambayo Yesu alizaliwa.
Chini ya agano la kale Mungu alihahidi afya njema na mafanikio kwa wale waliotii amri zake. Taifa la Israeli lilikuwa kuu na tajiri wakati walimtumaini Mungu. Wale Wayahudi waliorudi Israeli hawakujua ni kuwa kwa mwanguko wa Israeli agano la kali halikutekelezwa tena.
Wanaume na Wanawake wakuu katika Agano la Kale
Tumeongea kuhusu kipindi kirefu sana kwa kurasa chache tu. Lakini Bibilia imejaa na hadithi juu ya wanaume na wanawake wakuu wa Mungu unahitajika kuwajua. Hapa kuna orodha tunaanza nayo. Vile unaanza kusoma Biblia bila shaka utapata wengine tengeneza katika iyo orodha. Mbona tusianze na hii na vile muda utaendelea utaongeza kusoma, uongeze orodha yako ya wakubwa wa biblia. Hakikisha umeandika chini milango na vifungu utakapovipata ili uweze kuvipata wakati wowote unataka.
Tuanze!
Kabla hujaenda mbali ndani mwa kitabu hiki, sas unaweza kuwa wakati mwema kuangalia baadhi ya vifungu hapo juu au zozote zile ambazo dondoo zao umepewa. Inaweza kuwa zoezi kuu la kusoma kuangalia milango na mafungu iliyorejerewa.